Home

Dira

Shule za viktoria zinajitahidi kuwa mfano bora wa kuigwa ili kwenda sambamba na changamoto za nchi.

Maelezo ya dhima

  • katika shule za viktoria, tumewiwa kutoa elimu bora kwa watoto wote, pia kwa wale wanaoishi katika mazingira magumu.
  • Tunaamini katika udadisi, moyo uliowazi na watu wanaowajibika huchangia haki na Amani katika jamii.

Lengo / Dhamira

Tunajitahidi kuleta urafiki na mazingira chanya ya ujifunzaji, ambayo kila mtoto huhudumiwa kulingana na hitaji lake, wajibu pamoja na haki zake.

Kauli mbiu ya shule

Katika shule za viktoria tunatambua kwamba elimu bora ni ile isiyopimika thamani yake hii ndiyo sababu inayotufanya tujitahidi kutoa muda unaowafurahisha watoto wote pindi wawapo shuleni. Kulingana na kauli mbiu yetu “Daima tafuta Maarifa” Tunataka kuwapa motisha watoto kujifunza kwa kufuata uhuru wa matakwa yao katika maisha yao yote. Hivi ndivyo watoto wetu watakavyofanikiwa kwenye taaluma na maisha binafsi. Shule yetu hufundisha stadi za mawasiliano pamoja na ubunifu wa fikra. Kwa rasilimali hizi, kila mtoto anao uwezo wa kufikia kiwango cha juu cha taaluma.

Falsafa

Zaidi ya yote, jamii yetu inapitia mabadiliko, inahitaji mitazamo mipya na ongezeko la ufaulu kwa kila mmoja. Katika Viktoria, kila mtoto lazima apokee elimu iliyo imara. Hivyo basi tunajitahidi kuandaa mazingira chanya ya ujifunzaji ambayo kila mtoto huhudumiwa kulingana na hitaji lake, wajibu pamoja na haki zake. Hii huhitaji malengo pamoja na maadili ya jumla /pamoja. Muingiliano katika shule za viktoria hutambulishwa kwa nidhamu chanya. Tunaachana na adhabu zinazogusa mwili wa mtoto kama vile kuchapa pindi mtoto anapokosea. Miongozo yetu huendana na usawa kati ya mila desturi na maadili ya jamii ya Kitanzania. Tunaamini kwamba, udadisi, moyo uliowazi na watu wanaowajibika huchangia Haki na Amani katika jamii. Shule za Viktoria tunajitahidi kuwa mfano bora wa kuigwa ili kwenda sambamba na changamoto za nchi.

Ushirikiano

Tunafungamanisha umuhimu mkubwa wa mahusiano mazuri kati ya shule na wazazi. Pia ni muhimu kwetu kuanzisha mawasiliano ya wazi baina ya uongozi, wafanyakazi na jamii inayotuzunguka kwa mazingira chanya ya kiutendaji. Kwa mahusiano mazuri, tunaweza kutoa elimu bora kwa mwanao.

About

Ukubwa

Jumla ya Wanafunzi: 506
Wasichana: 249
Wavulana: 257
Jumla wa Wafanyakazi: 50
Walimu: 24
Wafanyakazi wasio Walium: 26

 

History

Waanzilishi na wakurugenzi wa Shule za Viktoria.

  • Switbert Rutinwa TIbandekile
  • Johanna Sele Rutinwa

Namna shule ilivyoanzishwa

Waanzilishi na Wakurugenzi wa Shule za Viktoria Bw na Bi Rutinwa mara kwa mara wamekuwa wakisimamia ubora wa shule na kuwa na mawasiliano chanya kwa wanafunzi. Ulipofika mwezi wa tisa mwaka 2010, wanandoa hawa waliona ni vyema kuwa na taasisi inayotoa elimu kwa watoto wadogo. Ndipo walipoamua kununua shule ambayo tayari ilikuwa inaendelea kutoa elimu kwa lugha ya kiingereza. Waliamini kwamba wakisomesha watoto, basi watakuwa wamechangia moja kwa moja kwenye maendeleo ya taifa hili kwa siku zijazo. Watoto wakisoma watakuwa na mchango mkubwa kwenye jamii zao kutokana na elimu watakayo kuwa nayo. Kwa kuzingatia hili na kutokana na taaluma walizonazo kama vile Ualimu na Ustawi wa jamii, Bwana na Bibi Rutinwa mwaka 2016 waliamua kukabidhi shule katika mikono ya (NGO) Viktoria Development Movers and Education Support Organisation.

Wafanyakazi

Waajiriwa na Wakurugenzi ni rasilimali wenye umuhimu mkubwa kwani kwa pamoja wanahusika pakubwa kwenye ufanikishaji na hata kufikiwa kwa malengo ya taasisi. Wakurugenzi wanasimamia maadili na kuyahuisha kwa wafanyakazi. Mahusiano mazuri baina ya wafanyakazi na waajiri yanaendelea kuwa bora zaidi kutokana na namna wanavyo heshimiana kila mmoja. Mazingira mazuri ya kazi pamoja na muendelezo wa utoaji semina za mara kwa mara kwa wafanyakazi juu ya nidhamu chanya ni muhimu sana.

Vifaa

Chumba cha kuhifadhia zana za kujifunza na kufundishia

Kwenye chumba hiki kuna kila aina ya zana za kujifunza na kufundishia. Walimu wetu mara zote huaandaa masomo yao kwa kutumia zana zinazopatikana ndani ya chumba hiki. Wakiwa darasani walimu hutumia zana zinazoibua hisia za wanafunzi juu ya somo husika, vitabu vyenye michoro na picha mbalimbali, filamu n.k. Matumizi ya zana hizi hufanya kipindi kivutie na kuongeza uchangamfu wa wanafunzi kwenye somo husika.

Chumba cha kompyuta

Chumba chetu cha kompyuta, kina kompyuta za kisasa, vifaa vya kisasa pamoja na programu za kisasa na intaneti. Chumba hiki kina kompyuta za mezani 45, kompyuta mpakato, vifaa vya usikivu pamoja na projecta mbili.

Maktaba

Lengo letu kubwa la kuwa na maktaba hii ni kuandaa mazingira mazuri ya wanafunzi wetu kufurahia usomaji wao. Maktaba hii huwavutia watoto katika usomaji wao wa vitabu mbalimbali vinavyohusiana na taaluma na maarifa mengine ya ziada. Ndani ya maktaba hii kuna vitabu vya hadithi, vitabu vya picha, riwaya, sayansi, vitabu vya kiada, majarida pamoja na kamusi. Ni ruksa kwa kila mtoto wa Viktoria kutumia maktaba hii.

Viwanja vya michezo

Imethibitika pasipo shaka kuwa “uwezo wa mtoto kusoma kwa kipindi kirefu hushuka kadri ya muda. Hivyo, ili awe na muendelezo mzuri wa usomaji anatakiwa apumzike, acheze, ajinyooshe na kisha kuendelea na masomo. Hapa shuleni wanacheza mpira wa miguu, kuruka kamba, kupumzika kwenye vivuli vyenye hewa safi na maua ya kupendeza.

Mazingira

Katika shule yetu tunasisitiza utunzaji wa mazingira yetu hali inayowafanya wanafunzi wetu wajisikie faraja. Bustani yetu inayopendeza imepambwa na rangi mbalimbali za maua kiasi cha kuvutia kutokana na mazingira yake chanya. Ina maeneo mengi ya wanafunzi kujisomea kuandika na hata kujadiliana juu ya masuala yahusuyo taaluma. Wanafunzi wanaweza kutumia jengo maalum la nje (kibanda), bwalo la chakula, au madarasa rafiki kujifunza na kupata maarifa mapya.

Syllabus

Chekechea na mfumo wa montessori

Umakini binafsi, heshima, kujali muingiliano na malengo sahihi humruhusu kila mtoto kuwa na mwanzo mzuri wa safari ya kielimu. Kwenye chekechea yetu, kila mtoto anayo nafasi ya kuendelea na kuitii kiu ya maarifa.

Ukweli kuhusu kauli mbiu ya Maria Montessori “Nisaidie niweze kufanya mwenyewe’’ Madarasa yetu mawili ya chekechea yanaendeshwa kitaaluma kwa kufuata dhana ya Montessori. Wanafunzi wote wanayo nafasi ya kuvumbua kitu kipya kupitia hisia zao na kujifunza kile walichokivumbua. Kila kinachowazunguka watoto huwapa ujuzi wa kujifunza maudhui kimwili na kiroho pia. Chekechea yetu inazo zana mbalimbali za kujifunzia hali inayomfanya mtoto awe na ubora wa kuanza darasa la kwanza.      

Ratiba za shule

Katika shule za Viktoria tunatoa Elimu inayojitosheleza kwa watoto wetu. Lugha yetu ya mawasiliano ni Kiingereza na tunafuata mtaala wa Tanzania. Tunawaanda watoto wetu ipasavyo kwa ubora wa sasa na hata baadae wanapojiunga na elimu ya sekondari. Zaidi tumeimarika katika kuwaandaa watoto kwa Maisha yao ya baadaye. Katika shule yetu, watoto ni lazima wawe na fikra tunduizi, waweze kujisimamia na kuyasimamia mawazo yao. Ni jukumu letu kuwafundisha watoto ili waweze kujiamini na kuakisi matendo ya kuigwa na watoto wenzao. Zaidi ya hapo, ni wajibu wetu mkubwa kuyaweka katika Matendo yale tunayoyafundisha na kuwaonesha watoto wetu umuhimu wake katika Maisha ya kila siku. Katika shule yetu tunafundisha stadi za Maisha pamoja na stadi za kijamii. Tumeshawishika kwamba stadi hizi ni ufunguo wa mafanikio katika maisha.

Mafunzo maalum

Sanaa na michezo

Kila siku ya ijumaa mchana tunakua tuaendesha kipindi cha Sanaa na michezo”. Wanafunzi wote wanagawanywa katika makundi madogo madogo na kisha kuendelea na kujishughulisha na mada/ mchezo husika chini ya usimamizi wa walimu husika.ofa zetu ni kubwa/nyingi na huwafanya watoto kuwa hodari na shupavu. Wanafunzi wana weza kupaka mengine mingi. Kwa hiyo tumemaliza wiki ya masomo ya ziada nje ya mtaala wa kawaida.

Siku maalum ya mazingira

Tunazingatia sana elimu jumuishi ya watoto wetu hapa shuleni. Hii ni pamoja na utambuzi wa asili na mazingira ambayo tunafikisha kwa watoto wetu wote. Hivyo kwa kila mwezi tunatumia vipindi viwili vya masomo ya darasani kufanya usafi wa mazingira ya shule. Kwanza, watoto wanaandaliwa kinadharia na kisha kujumuika kwenye shughuli za usafi wa bustanini na mazingira kwa ujumla. Kwa kuwa miti ilishapandwa na maua nayo kuoteshwa, uokotaji wa taka pamoja na usafi wa madarasani pia ni sehemu ya somo. Kwa jinsi hii, watoto hujifunza namna ya kutunza mazingira na asili yake kwa heshima na endelevu. Kama zawadi, siku hii tunakula pilau, nyama na matunda kama chakula cha mchana pindi tu tunapomaliza kazi ya usafi; hali hii humfurahisha kila mtoto.

”Kujihami” na “Amani Ni Maamuzi” (PiaD)

“Stadi za Maisha” vipindi vya usawa na heshima navyo pia ni muhimu katika mazingira ya ujifunzaji.

Kujihami

Katika kipindi hiki cha kila wiki tunawafundisha watoto wetu wa kike namna ya kuishi kwa kujiamini, kujilinda, kujithamini na kuongelea umuhimu wa kuwa na malengo katika Maisha. Tunawaelekeza namna ya kujilinda kimwili na kwa maneno, pia kipindi hiki hujenga mshikamano kwa makundi mbalimbali ya wasichana na kumuimarisha mtoto wa kike kwa Maisha yake ya kila siku na yajayo pia.

Amani Ni Maamuzi (PiaD)

Wasichana wanapoendelea na mafunzo ya kujihami, wavulana pia tunawaelekeza namna ya kutatua migogoro mbalimbali kwa njia ya Amani. Tunazungumza nao umuhimu wa kuwachukulia sawa, kuwajali na kuiheshimu jinsia ya kike kwa ujumla pamoja na namna ya kuandaa malengo na kuyatimiza pia. Kwetu ni muhimu kuandaa jamii inayosimamia Amani na siyo machafuko au vurugu. Pia imewahi kuthibitishwa kwamba kuchangamana kwa njia ya Amani huchangia mazingira bora ya ujifunzaji na usomaji.

Class teachers hour

Hutoa muda wa maridhiano miongoni mwa wanafunzi na walimu. Ni muda mzuri wa kujadili msitakabali wa maendeleo ya darasa husika kitaaluma na kijamii.

Ofa zetu

Usafiri

Kila asubuhi mabasi yetu matatu ya shule huwafuata watoto majumbani kwao na kuwaleta shuleni. Muda wa masomo unapokwisha, watoto hurudishwa nyumbani kwa mabasi hayo yanayoendeshwa na madereva wetu waaminifu na mahiri.

 

Chakula Na Lishe

Kila saa nne asubuhi tunapata uji wa lishe ulioandaliwa vizuri na wapishi wetu watatu. Kwa upande wa chakula cha mchana, tuna aina ya vyakula mbalimbali kila siku. Kwa mfano mara moja kwa wiki watoto wetu hula wali maharage pamoja na matunda mbalimbali kama vile tikitimaji, ndizi, machenza, machungwa n.k. Kingine kinachoifanya shule yetu kuwa tofauti na shule nyingine ni uwepo wa maji safi na salama ya kunywa muda wote. Watoto hupata maji safi na salama ya kunywa muda wote.

Uchunguzi wa kiafya

Kila mwaka wanafunzi wetu hufanyiwa uchunguzi wa kiafya na madaktari waliobobea katika hospital iliyo jirani na shule yetu ya Mt. Clare. Hapa wanafunzi wote ambao wazazi wao wamehiari; hufanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kisha wazazi hupewa majibu. Uchunguzi huu umekuwa na mafanikio makubwa kwani wanafunzi baadhi wamegundulika kuwa na tatizo la uoni hafifu pamoja na magonjwa mengine. Tunaamini kwamba msingi wa kwanza wa matokeo mazuri ya shule ni afya na uimara wa mwili wa mtoto. Kama tunavyojua, afya ni kitu cha msingi na muhimu sana katika Maisha yetu.

Ziara ya kimasomo

Kama shule tunatoa motisha kwa wanafunzi wetu kwa kuwapa zawadi hasa wale wanaofanya vizuri kitaaluma. Kwa kweli, hili tunalifanya kielimu zaidi kwa mfano, kila mwaka tunafanya ziara za kimasomo kwenye mbuga za Serengeti, Ngorongoro, Manyara, Saanane na Makumbusho ya Kihistoria kama vile Bujora na maeneo mengine yanayovutia. Ziara hizi huandaliwa na shule kwa kushirikiana na wanafunzi. Wanafunzi wanapata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali kuhusiana na maeneo husika, kubadilishana mawazo na walimu pamoja wafanyakazi wakiwa kwenye maeneo tulivu. Hali hii huimarisha mauhusiano baina ya wanafunzi, wafanyakazi na walimu wao.

Matukio

Mwezi wa tisa kila mwaka tunakuwa na mahafali ya shule. Mahafali haya hufanyika hapa shuleni kwenye bwalo letu linalovutia kwa rangi na mapambo ya aina yake. Kwenye tukio hili tunaalika familia, ndugu na marafiki ambapo kunakuwepo na hotuba, maonesho na burudani mbalimbali. Tunafurahia chakula cha mchana pamoja na keki maridhawa na vinywaji mbalimbali. Hili kwetu ni tukio muhimu la kuwaaga wapendwa wetu wa darasa la saba kwa kuwatakia kila kheri katika safari yao ya kujiunga na Elimu ya Sekondari.

Mabweni

Uwepo wa mabweni huwapa wanafunzi nafasi ya kuzoeana kitabia, kijamii na kitamaduni kwa kuwa pamoja muda wote. Hutoa nafasi kwao kuendeleza stadi za Maisha na kutengeneza urafiki wa kudumu. Mabweni yetu ni mahali salama ambayo wanafunzi hujisikia Amani, furaha na hata kusaidiana kimasomo. Huwapatia watoto msaada unaohitajika katika maisha yao ya kila siku wanapokuwa shuleni na kuwaandaa kwa maisha yao ya baadae.

Nukuu mbalimbali /Taarifa

Motisha Walimu - Wanafunzi wenye furaha

Usaili

Tunapokea wanafunzi wapya kuanzia elimu ya awali hadi darasa la (vii).

Test and Interview

Kwa madarasa ya awali hakuna jaribio au usaili wowote unaotolewa kwa mtoto.

Kwa madarasa ya kwanza (I) na pili (II), mwanafunzi hufanyiwa usaili kwenye masomo matatu ambayo ni kiingereza, Kiswahili (kusoma) na hesabu.

Kuanzia darasa la tatu (III) hadi la saba (VII), mwanafunzi hupewa masomo yote kwa ajili ya usaili.

Nyaraka zinazotakiwa (Taarifa muhimu)

Mzazi anawajibika kuleta nyaraka zifuatazo

  • Cheti cha kuzaliwa.
  • Picha 1 ya pasipoti.
  • Fomu ya uhamisho.

Namba ya akaunti

Malipo yote ni kwa shillingi za kitanzania.

CRDB
Viktoria English medium schools (Shule za michepuo ya Kiingereza Viktoria
Namba ya akaunti: 0150016789400
S.W.I.F.T. Msimbo; CORUTZTZ.